Serikali imesema mradi wa ujenzi wa jengo la abiria la tatu umekamilika kwa asilimia 66 na kwamba mradi huo utakamilika Septemba, mwakani kama ilivyopangwa kwa kuwa kwa saasa hakuna kikwazo chochote.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Elias Kwandikwa wakati alipotembelea mradi huo leo, jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa serkali imeshamlipa mkandarasi fedha anazodai na kwa sasa hawana deni.
"Awamu hii ya pili tunajenga uwanja huu kwa fedha zetu za ndani, hii ni ishara tunaelekea kuzuri kwamana itafika mahali tutakuwa na miradii kama hii kwa fedha zetu wenyewe," amesema Kwandikwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni