Maelfu ya raia wa Australia yaandamana kupinga unyanyasaji wanaotendewa wakimbizi nchini Australia.
Waomba hifadhi nchini Australia katika kambi ya wakimbizi inayopatikana katika kisiwa cha Manus Papua New Guinea walikusanyika na kupinga unyanyasaji wanaotendewa.
Umoja wa Matifa amesema kuwa wakimbizi katika kisiwa hicho wapo katika hali ya dharura na wanahitaji msaada.
Wahamiaji hao wamesema kuwa wanahofia maisha yao kuondaka katika kambi waliokuwa wamezuiliwa na Australia. Kambi hiyo ilifunga Jumanne na huduma zote kufungwa.
Vyombo vya habari vimesema kuwa maji , umeme na chakula hakuna katika kambi hiyo iliofungwa na serikali ya Australia.
Tangu mwaka 2012 serikali ya Australia ilichukuwa hatua ngumu dhidi wa wahamiaji na kuwazuaia katika kisiwa cha Manus Papua New Guinea na Nauru.
Kwa mujibu wa taarifa zilzitolewa na Umoja wa Mataifa, wakimbizi 900 wamezuiliwa kama wafungwa katika kisiwa cha Manus, 12 000 katika kisiwa cha Nauru.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni