Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeteketeza nyumba moja katika eneo la Ubungo kwa Mbonde asubuhi hii.
Wananchi wa eneo hilo waliendelea na jitihada za kuzima moto huo, lakini kutokana na kuwa mkubwa zaidi jitihada hizo zilishindikana.
Tayari kikosi cha jeshi la zimamoto kimewasili eneo la tukio ili kuzima moto huo pamoja na mafundi wa umeme kutoka Tanesco kitengo cha dharula ili kukata umeme kuzuia madhara zaidi.
Bado hakujatolewa taarifa yoyote ya vifo au majeruhi, EATV itaendelea kukuletea taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika.
Endelea kubaki nasi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni