Jumanne, 7 Novemba 2017

Nikki wa Pili afanya kolabo na Waziri Njenje kutoka Kilimanjaro Band

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili amezungumzia kolabo yake na Waziri Njenje kutoka Kilimanjaro Band.

Rapper huyo wa kundi la Weusi amesema kazi hiyo kuna sehemu fulani imeshafika hivyo watu wakae mkao wa kula.

“Kwa sasa siwezi kusema wazi nitaharibu lakini kuna kitu fulani nilikuwa nimefanya ambacho nilipata inspiration kutoka kwa kwenye muziki wa Njenje, nikakutana na mzee Waziri Njenje nikamsikilisha akakielewa, kwa hiyo kutoka pale tukakipeleka next level, kwa hiyo ni kitu gani na nini watu wa-stay tune” Nikki ameiambia Bongo5.

Waziri Njenje pamoja na wenzake wameshafanya kolabo na baadhi ya wasanii wa Bongo Flava kama Mwana FA ‘Kama Zamani’ na Kassim Mganga ‘Somo’.

Hakuna maoni: