Umoja wa Vyama vya upinzani nchini Kenya, NASA umeandaa Kongamano siku ya Jumanne tarehe 28 Novemba 2017, siku ambayo Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa.
Kongamano hilo lina lengo la kuwaombea watu wote waliopoteza maisha na wale waliopata ulemavu katika kipindi cha Uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kongamano hilo litafanyika katika viwanja vya Jacaranda eneo la Embakasi jijini Nairobi. ambapo hadi sasa Maafisa wa polisi mjini Nairobi wamesema hawajapata taarifa yoyote juu ya kongamano hilo.
”Hatujui kwamba kuna mkutano kama huo.hatujaarifiwa. Kwa hivyo mtu yeyeto ambaye anadhani anaweza kufanya mkutano mkutano huo bila kuarifu polisi, mwambieni mtu huyo kwamba sheria itakabiliana na hali hiyo.“amesema msemaji wa jeshi la polisi mjini Nairobi, Japhet Koome kwenye taarifa iliyotolewa jana kwa Waandishi wa Habari.
Hayo yanajiri katika kipindi ambacho tayari viongozi wa upinzani nchini Kenya wakisema kuwa hawautambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.
Kiongozi wa NASA Taifa, Musalia Mudavadi amesema kuwa watatumia njia halali zilizopo kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta licha ya kuidhinishwa na mahakama ya juu.
Mudavadi amewaambia Wakenya kutohudhuria katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Kasarani siku ya Jumanne na badala yake kuhudhuria katika kongamano la upinzani huo ili kuomboleza mauaji ya waathiriwa waliouawa na maafisa wa polisi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni