Naibu waziri wa maji na umwagiliaji, Mhe. Jumaa Awesso amewaonya watendaji wa mamlaka za maji hapa nchini kuacha mara moja tabia kuwabambikia bili kubwa ya maji wananchi kwa makusudi na kwamba serikali ya awamu ya tano haipo kwa ajili ya kuwanyanyasa wananchi wake na imejipanga vyema kuhakikisha inatatua kero ya maji kwa wananchi tofauti na ilivyokua mwanzo.
Onyo hilo la naibu waziri wa maji na umwagiliaji, Mhe.Jumaa Awesso amelitoa mara baada ya wananchi wa Ruhila mjini Songea mkoa wa Ruvuma kutoa malalamiko ya kupewa bili za maji kubwa kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SOUWASA) mkoa wa Ruvuma jambo ambalo naibu waziri huyo wa maji amesema tabia hiyo imeanza kuibuka kwa baadhi ya mamlaka za maji na akatoa onyo kwa watendaji wote wa mamlaka hizo kuacha mara moja tabia hiyo.
Pamoja na kuwepo kwa malalamiko hayo lakini pia wananchi wa Seed Farm Songea waliopisha ujenzi wa mradi wa maji katika bonde la mto Ruhila Songea wameilalamikia serikali kuchelewa kuwalipa fidia zao kwa zaidi ya miaka 14 sasa huku Mhe. Jumaa Awesso akiwapa matumaini wananchi hao kwamba fidia yao watalipwa.
Aidha naibu waziri huyo wa maji ametembelea na kukagua vyanzo mbalimbali vya maji mjini Songea na kuwahakikishia wananchi kwamba serikali imedhamiria kutatua kabisa tatizo la maji katika miji 17 hapa nchini ikiwemo Songea kupitia fedha kutoka nchi ya India zaidi ya dola 503.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni