Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limempokea Mwanazuoni Mkubwa wa Kidunia , Abib Omar Bin Hafith kutoka nchini Yemen ambaye atakuwepo nchini kwa ziara ya siku mbili.
Akizungumzia ujio huo Mufti Mkuu wa Tanzania ,Sheikh Abubakar amesema mambo atakayofanya mwanazuoni huyo ni pamoja na kuiombea nchi iendelee kuwa na amani na upendo.
"Tulimuomba kwa zaidi ya miaka miwili mwanazuoni mkubwa wa kidunia aje nchini na tunashukuru ametukubalia ombi letu hivyo tutayapokea yale yote aliyotuletea" amesema Sheikh Abubakar.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amesema kuja kwa mwanazuoni huyo ni ishara ya upendo na amani ambapo nchi mbalimbali walikuwa wanamuhitaji lakini ameona aje nchini kutembelea
Imam wa msikiti wa Shibu uliopo Mombasa nchini Kenya, Izudin Alwy amesema wanayo furaha kubwa hivyo wamejiandaa kupokea yale ambayo watapewa ili waweze kuyafanyia kazi.
"Sisi tumejiandaa kuyapokea na tutafaidika na yale ambayo mwanazuoni huyo amekusudia kutupa," amesema Imam Alwy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni