Jumatatu, 27 Novemba 2017

Mwanamfalme Harry kumuoa mpenzi wake Meghan Markle


Mwanamfalme Harry atamuoa mpenzi wake ambaye ni muigizaji nchini Marekani Meghan Markle, kasri la Clarence Uingereza limetangaza
.
Mwanamfalme huyo ambaye ni wa tano katika orodha ya ufalme atamuoa Bi Markle msimu ujao wa machipuko na wataishi katika kasri la Kensington mjini London.

Wapenzi hao ambao wamekuwa wakichumbiana tangu Julai mwaka 2016 na Harry alimposa Meghan mwezi wa Novemba.

Ni malkia na "jamaa wengine wa karibu katika familia yake" ndio waliojua kuhusu uposo huo awali uliofanyika London.

Mwanamfalme Harry athibitisha mpenziwe

Prince Harry akutana na Rihana Barbados

Mwanamfalme Harry amesema " ana furaha kutangaza" uposo huo na kwamba amepokea baraka za wazazi wa Bi Markle.

Wachumba hao walionekana mbele ya umma pamoja kwa mara ya kwanza mnamo Septemba.

Hakuna maoni: