Jumanne, 21 Novemba 2017

MECHI ZOTE ZA LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA (UEFA)

Image result for dortmund vs tottenham 2017
Ligi ya mabingwa barani Ulaya itaendelea usiku wa leoJumanne Novemba 21,2017 kwa Mechi za kundi E,F,G na H kuchezwa katika viwanja mbalimbali barani humo.

Kundi E wenyeji Sevilla kutoka Spain wataialika Liverpool toka nchini England wakati Spartak Moscow wao watakua nyumbani kumenyana na Maribor. 
Kwenye kundi hili hakuna timu iliyopata nafasi ya kusonga mbele mpaka sasa kwani Liverpool wanaongoza wakiwa na pointi 8 huku Sevilla wakiwafatia wakiwa na pointi 7 wakati Spartak Moscow wao wana pointi 5 huku Maribor wakishika mkia na pointi yao 1 hivyo kufanya timu mbili kati ya hizo tatu za mwanzo kila moja kuwa na nafasi ya kusonga mbele.
Kundi F Vinara wa ligi kuu ya England hivi sasa Manchester City wao licha ya kuwa wameshafuzu kwa hatua inayofuata watakua nyumbani kuwakaribisha Fayernoord ya Uholanzi wakati Napoli wataialika Shaktar Donetsk ya Ukraine.
Kundi G litashuhudia vinara wa kundi hilo Besiktas ya Uturuki wakiialika FC Porto ya Ureno wakati RB Leizpig ya Ujerumani watakua wageni wa Monaco ya Ufaransa.
Group H ambalo lilionekana kama kundi la kifo wenyeji APOEL Nicosia watawakaribisha Real madrid ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wakati Tottenham Hotspurs itasafiri mpaka Ujerumani kuivaa Borussia Dortmund 
MECHI ZOTE HIZO ZITAANZA SAA 5 KASOROBO USIKU ISIPOKUA MECHI MOJA BAINA YA SPARTAK MOSCOW NA MARIBOR ITAKAYOANZA SAA 2 KAMILI USIKU


Hakuna maoni: