Jumapili, 26 Novemba 2017

Maalim Self amvaa profesa Lipumba

 Na. Ahmad Mmow. 
ALIYEWAHI kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na katibu mkuu wa CUF, Maalim Self Sharrif Hamad amesema chama hicho hakina mgogoro wa ndani ya chama hicho umetengenezwa na dola kwa kumtumia profesa Ibrahim Lipumba ili kuuwa upinzani.

Maalim alisema hayo leo wakati wa mkutano mkuu wa wilaya wa chama hicho uliofanyika leo katika mamlaka ya mji mdogo ya Kilwa Kevinje wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.

Alisema mgogoro uliopo ndani ya chama hicho umetengenezwa na dola kwa kumtumia profesa Ibrahim Lipumba ili kuuwa upinzani na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umekuwa tishio kwa Chana tawala. Alisema wakati CUF kikiwa kimepandikiziwa mtu wa kukivuruga, CHADEMA kinashugulikiwa kwa mtindo mwingine.

Maalim alisema mkakati wa kuuwa upinzani na Umoja wa Katiba ya Wananchi ulianza kabla ya uchaguzi ili aondoke na wanachama wakati anajiuzulu nafasi ya uenyekiti. Hata hivyo hakuna aliyemfuata.

"Alipoona mkakati huo haukuanikiwa akaamua kulazisha kurudi, Ingawa alikaa nje kwa miezi kumi. Hii haijawahi kutokea duniani, ila Lipumba amefanya, "alisema Maalim Self.

Maalim anaetajwa kuungwa mkono takribni na wabunge wote wanaotokana na chama hicho, alisema profesa Lipumba hakuondolewa kwenye nafasi hiyo bali aliondoka mwenyewe na mkutano mkuu uliiridhia kujiuzulu kwake.

" Tunajua hata tiketi alikatiwa nanani, alisindikizwa na nani nakule alikokwenda alipokelewa nanani, "Seif alizidi kuvaa profesa.

Kama hiyo haitoshi mwanasiasa huyo anaetajwa kuwa naushawishi mkubwa kisiasa ndani na nje ya nchi alisema nijambo la kushangaza kuona profesa huyo wa uchumi anapambana kukiuwa alichokiasisi mwenyewe. Huku akifafanunua kuwa mwanzilishi wa UKAWA ni profesa Lipumba. Kwamadai umoja huo ulianza kwenye bunge la Katiba. Ambapo licha ya profesa kuwa mjumbe wa bunge hilo, bali ndiye aliyetoa wazo la kuanzisha umoja huo.

Mbali na hayo  alisema hata Edward Lowassa anaemtaja kuwa alimkimbia alimtafuta na kumuingiza katika UKAWA. kwamadai kwamba ni yeye alimtetea baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu Lowassa kuhusishwa na ufisadi.

"Nihuyohuyo aliyasema hakuwa fisadi, bali ufisadi ulikuwa ni mfumo wa CCM, wa Tanzania waelewe mgogoro ndani ya CUF-Chama Cha wananchi umepandikizwa na dola, "alisisitiza Maalim Self.

Katika hali iliyoonesha alikuwa ameamua kutumia nafasi hiyo kutapika nyongo, mwanasiasa huyo mkongwe alisema madai kusema Dkt Wilbroad Slaa ndiye alistahili kugombea Urais kupipitia UKAWA tayari yamepata mujibu. Kwasababu ameteuliwa na serikali ya Chama  Cha Mapinduzi kuwa balozi.

Kwaupande wake mbunge wa jimbo la Tumbe, Rashid Ally alisema chama hicho  na wapenda utawala wa sheria wanasubiri kuona spika wa bunge atafanya nini baada ya wabunge na madiwani waliofukuzwa na profesa Lipumba, lakini mahakama imesema bado wanaendelea kuwa wanachama hadi kesi ya msingi iliyofunguliwa na chama hicho itolewe uamuzi.

Wakati spika amewaapisha  wanachama wengine wachama hicho ambao alipelekewa na tume ya uchaguzi.




Hakuna maoni: