Jumapili, 26 Novemba 2017

LIBYA: WAHAMIAJI HARAMU 31 WAFARIKI BAADA YA MASHUA YAO KUZAMA

Wahamiaji haramu 31 wafariki na wengine 35 waokolewa baada ya mashua yao kuzama katika  pwani ya Libya

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na polisi ya pwani ya Libya ni kwamba wahamiaji haramu 31 wamefariki na wengine 35  wamokolewa baada ya mashua yao kuzama nchini Libya.

Msemaji wa polisi ya kulinda pwani Libya kanali Ayub Qassem amefahamisha Jumamosi kuwa  operesheni ya kuwaokowa wahamiaji hao ilifanyika katika eneo la Castelverde Mashariki mwa Tripoli.

Kanali huyo amefahamisha kuwa miongoni mwa watu waliookolewa walikuwemo  watoto.



Hakuna maoni: