Matola aliyasema hayo leo mara baada ya Klabu anayoifundisha,Lipuli Fc kuibana mbavu Simba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliochezwa leo Jumapili novemba 26, 2017 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.
"Mimi ni Simba , Hamna mtu asiyejua kwamba mimi ni Simba,Nimecheza simba kwa muda mrefu,nimefundisha lakini unapokuwa kwenye kazi lazima uangalie kazi"
Awali akiuzungumzia mchezo huo matola alisema kilichosababisha wasifungwe kwenye mchezo huo ni mbinu aliyoitumia ambapo timu yake ilijikita zaidi katika kulinda goli ili maadui wasipate nafasi ya kushambulia.
"Nilitaka nizuie sana kwenye eneo la golini ili Simba wasiweze kumfikia golikipa kwa karibu na ndicho ambacho nilichohitaji"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni