Na Faridi Miraji
Baada ya mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hanspope kumtolea uvivu kuhusu majeraha yake
Mwenyekiti huyo ambaye huwa anaongea ukweli amesema
"Inategemea na yeye mwenyewe Kama anataka kucheza acheze Kama hataki aende, ni muoga sana.Msimamo ni yeye mwenyewe aamue Kama anacheza acheze Kama hataki aende, vipimo havidanganyi kwani vinaonesha tayari amepona "
"Sisi hatuwezi kumsajili mchezaji kwa pesa nyingi harafu hachezi, tumeshindwa kumvumilia "
Amesema Hans Pope
Klabu ya Simba Sc ilimsajili mlinzi huyo toka Azam FC katika usajili uliopita ila alipata majeraha ya July 15 kwenye mechi ya Taifa Stars dhidi ya Rwanda kwenye harakati za kufuzu CHAN mchezo uliochezwa Jijini mwanza katika Dimba la ccm kirumba Mpaka sasa Shomary Kapombe hajawahi kuitumia klabu yake hiyo mpya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni