Jumanne, 28 Novemba 2017

HAJI MANARA ACHOKA,ATAJA MAMBO 2 YANAYOMKERA SIMBA




Afisa habari wa Klabu ya Simba ameonyeshwa kukerwa na Baadhi ya washabiki ambao wamekuwa wakimsumbua sana kuhusiana na Mambo mawili ndani ya Klabu hiyo inayotokea Mitaa yamsimbazi Manara ameongea kuhusiana na Washabiki kutaka kila timu inapocheza ishinde na siyo matokeo mengine na Suala la Kuambiwa kuwa yeye anamtetea sana omog

Akiongea kuhusu watu kutaka matokeo ya Ushindi pekee, Manara amesema
” Najiuliza mara mbili mimi kwanza  natosha? maana labda mimi sijui  sidhani kama kuna mtu anayeumia kama mimi maana mimi ndiye nashambuliwa, natukanwa, nachorwa katuni, nakashifiwa lakini kuna muda najiuliza tunakwenda wapi? inamaana watu hawataki matokeo yoyote lazima ushinde? “

Akiongea Kuhusu OMOG
Haji Manara amesema anaumizwa kuhusu tabia ya baadhi ya washabiki ambao wanamwandikia kwenye mitandao ya Kijamii kuwa anamtetea sana Omog jambo ambalo huwa anatakiwa azungumzie mambo ambayo anaagizwa na Uongozi kusema.
” Kuna wakati watu wengine wanaandika kwenye mitandao ya kijamii unamtetea sana Omog, kazi yangu mimi si kumtetea au kumpuuza yeyote kazi yangu kutumwa na Viongozi katangaze fulani tumemsimamisha, fulani tumemfukuza,fulani tumemsajili ndo utaratibu wa kazi yangu “

Manara pia  amesema kuna muda inafikia mchezaji aliyecheza mchezo kwa mfano dhidi ya Lipuli anampa pole kwa matokeo waliyoyapata wakati alitakiwa yeye ndiyo atoe Pole kwao


Hakuna maoni: