Jumatatu, 20 Novemba 2017

ELIAS MAGULI ATAJWA USAJILI WA MSHAMBULIAJI YANGA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na mfungaji wa bao la kusawazisha la Taifa Stars dhidi ya Benin kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika hivi karibuni baina ya Benin na Taifa Stars Elias Maguli ametajwa kama mmoja wa nyota watakaosajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Habari ambazo uongozi wa Yanga umeshindwa kuzikaanusha wala kuzikubali zinasema mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Stand United atasaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa hao wa soka la Tanzania bara endapo makubaliano yatafikiwa.

Elias Maguli kwasasa anaichezea klabu ya Dhofar FC inayoshiriki ligi kuu ya Oman na anaonekana ni mtu sahihi kuweza kutibu ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga baada ya Donald Ngoma na Amiss Tambwe kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.


Hakuna maoni: