Na. Ahmad Mmow.
MBUNGE wa jimbo la Kilwa Kusini, Seleman Bungara (Bwege) ameonya kuwa vyama vya upinzani vitaendelea kushindwa kwenye chaguzi iwapo havitaacha ubinafsi.
Bwege ameyasema hayo leo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko alipozungumza na Muungwana kuhusu matokeo ya uchaguzi wa madiwani uliofanyika jana.
Bwege ambae pia ni mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kilwa alisema itakuwa ni ndoto vya upinzani kuking'oa Chama Cha Mapinduzi iwapo vitaendelea kuwa na tabia ya ubinafsi kwa kila chama kushiriki uchaguzi kivyake. 4:Alisema kama vyama hivyo visipojitathimini na kukubali ukweli kwamba njia pekee ya kukabiliana na CCM ni kuunganisha nguvu zapamoja, vitegemee kukiondoa madarakani.
Bwege alisema ukweli wa hilo umethibitika katika uchaguzi huo uliomalizika jana ambao CCM kimekomba karibu viti vyote.
Mbunge huyo alitolea mfano kata mojawapo iliyopo katika manispaa ya Mtwara ambayo aliyekuwa mgombea wa udiwani kupipitia chama hicho aliambulia kura 21 tu.Tena Alisa amenadiwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho,profesa Ibrahim Lipumba.
" Alikwenda Lipumba kumnadi, mbunge wa jimbo na viti maalumu wote wapo kambi yake. Lakini mgombea wao amepata kura ishirini na moja, kwamba mtaa anaoishi hakuna wanachama walau thelathini ni maajabu. Lipumba ndie anaesema hataki UKAWA, labda sasa atakuwa ameanza kupata majibu," alisema Bwege.
Bwege aliongeza kusema kwamba chama kimoja kimoja hakiwezi kuhimili vitimbi, vitisho na nguvu za CCM, kwahiyo viongozi na wanachama wake watendelea kuteseka wakati wa chaguzi lakini mwisho wa siku wanajikuta wanashindwa vibaya. Huku akitahadharisha kuwa hali hiyo ikiendelea watawakatisha tamaa Wananchi wanaoviunga mkono vyama hivyo.
Katika mkoa wa Lindi kata za Mnacho na Chikonji zilishindaniwa katika uchaguzi uliofanyika jana. Ambapo CCM kimeshinda viti vyote.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni