Jumapili, 26 Novemba 2017

Arsenal yashinda, yarudi 'Top Four'

Alexis Sanchez amefunga penalti katika muda wa kuyoyoma na kuipa Arsenal ushindi dhidi ya Burnley uwanjani Turf Moor.

Ilikuwa ni marudio ya mechi ya msimu uliokwisha kati ya timu hizo mbili uwanjani Emirates wakati raia wa Chile - Sanchez alipofunga bao kunako dakika 98 kushinda mechi hiyo.

Ilikuwa pia ni mara ya tatu mtawalia kuwa Gunners imepata ushindi katika muda wa mwisho wa mechi dhidi ya Clarets.

Pointi tatu iliyojinyakulia Arsenal inaikweza timu hiyo hadi katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi na hiyo ni baada ya jana Liverpool na Tottenham kushindwa kupata ushindi kwenye michezo yao.

Matokeo hayo yalikuwa ni pigo kwa upande wa Sean Dyche ikiwa wamefanikiwa ushindi wa mechi zao mpaka sasa huku wakionekana kama watanyakuwa pointi moja, lakini refa Lee Mason alitoa penati kwa Arsenal baada mlinzi James Tarkowski kumsukuma Aaron Ramsey.

Petr Cech ndiyo aliyekuwa na kibarua kigumu kati ya makipa wawili , akifanikiwa kuokoa mikwaju miwili na kumnyima goli Johann Berg Gudmundsson.

Hakuna maoni: