Mwanamke mmoja wa Uingereza ambaye anashikiliwa nchini Misri kwa kuingiza madawa ambayo yametajwa ni ya kutuliza maumivu akimpelekea muwe wake anayeishi Misri, huenda akahukumiwa miaka 25 jela au akahukumiwa kifo.
Laura Plummer mwenye umri wa miaka 33, alikamatwa Oktoba 9 mwaka huu baada ya vyombo vya usalama kugundua amebeba dawa aina ya tramadol na naproxen kwenye begi lake, ambazo alidai ni kwa ajili ya mume wake Omar raia wa Misri, aliyekuwa na maumivu ya mgongo kutokana na ajali.
Mama mzazi wa Laura Roberta mwenye miaka 63, dada yake Rachel mwenye miaka 31 na Jayne mwenye miaka 40 walimtembelea Laura akiwa gerezani nchini humo, na kusema kwamba ndugu yao anaishi maisha ya tabu gerezani, na wameambiwa huenda akahukumiwa miaka 25 jela au kifo kufanywa mfano kwa wengine.
Wanafamilia hao wameendelea kusema kwamba dawa alizobeba ndugu yao za tramadol ni sawa na dawa za kutuliza maumivu, lakini kwa Misri ni sawa na heroin kitu ambacho kimewashangaza zaidi.
Idara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, na kusema kwamba wanamuunga mkono Laura na familia yake juu ya kushikiliwa kwa ndugu yao huyo nchini Misri.
Sky News
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni