Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Dar Young Africans ,leo walikua uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya KMC(Kinondoni Municipal Council) inayoshiriki ligi daraja la Kwanza.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex-Chamazi majira ya saa moja jioni umemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Vijana wa KMC wnaonolewa na Felix minziro walionekana kujiamini zaidi upande wa ulizni na kuweza kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga.
Awali uongozi wa Yanga ulisema mapatao ya mchezo huo yatatumika kukarabati uwanja wa Kaunda ambao unamilikiwa na klabu hiyo uliopo pale Jangwani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni