Jumanne, 3 Oktoba 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AWATAKA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI KULIOMBEA TAIFA

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaomba waimbaji wa nyimbo za dini kuendelea kuliombea taifa ili amani izidi kudumu.

Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa ombi hilo leo alipokutana na kuongea na Uongozi wa kwaya ya Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mijuhu Dayosisi ya Kati Singida, ofisini kwake leo mjini Dodoma.

Waziri Mwakyembe amewapongeza kwa uimbaji wao na kuwaomba kuendelea kutunga nyimbo zenye ujumbe wenye kuliombea taifa na kudumisha amani.

Kwaya ya Furahini iliwakilishwa na Mwenyekiti wake Benjamini Ng’imba pamoja na mlezi wa kwaya hiyo Zakayo Munyawi ambao wametumia fursa hiyo kumweleza Waziri changamoto wanazokutana nazo kwenye uuzaji wa kazi zao ikiwemo wizi wa kazi hizo.



Hakuna maoni: