Mwanafunzi wa Shuleya Msingi Mwaya iliyopo Wilayani Ulanga mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kuvamiwa na mamba wakati akioga pamoja na wanafunzi wenzake mtoni.
Akizungumza na ITV Diwani wa kata ya Mwaya na diwani wa Kata ya Chirombolo wamesema matukio hayo yamekithiri zaidi katika kata hizo mbili hali inayopelekea wakazi wa kata hizo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kuhofia kuvamiwa na mamba na kulazimisha wakazi wengi kulala mapema.
Kwa upande wao viongozi wa Wilaya ya Ulanga wakiwamo madiwani katika Halmashauri ya Ulanga, wanasema wameandaa mpango mkakati wa kuweza kudhibiti kero hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni