Kulia ni koocha Mkuu wa Singida United, Hans van Der Pluijm |
Pluijm amesema, mechi tano walizocheza hadi sasa zimempa mwanga kumuonyesha kuwa anakikosi imara ambacho kinaweza kutimiza malengo ambayo wamejipangia.
“Safari bado ni ndefu lakini sioni sababu ya kushindwa kupata ushindi kutokana na idadi ya mechi ambazo tumecheza na kiwango ambacho kimeonyeshwa na vijana wangu,”amesema Pluijm.
Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema kila mechi kwao watacheza kama mchezo wa fainali hivyo hawatoidharau timu yoyote hata kama haina jina kama ilivyo kwa Simba na Yanga.
Amesema uzuri wa timu yake wanacheza bila presha, na ndio maana wanacheza vizuri na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zao.
Azam inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 10, baada ya kucheza mechi tano ambapo imeshinda tatu kupoteza moja na sare moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni