Dkt. Meru ambaye ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya viwanda na uwekezaji, aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Dkt. John Magufuli, Disemba 2015 na amehudumu katika nafasi hiyo hadi alipostaafu Jumatano wiki iliyopita.
Akizungumza katika hafla ya kumuaga Dkt. Meru, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage licha ya kumpongeza kwa kumaliza salama utumishi wa umma, alimsifu kwa umahiri wake wa kutekeleza sera ya maendeleo ya viwanda.
“Sote tunafahamu Serikali ya Awamu ya Tano inaamini katika viwanda, wewe ulikuwa mstari wa mbele katika kubuni mbinu na mikakati ya kuharakisha ujenzi wa viwanda nchini,” alisema Mwijage.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni