Jumatano, 4 Oktoba 2017

Hii kali, Kuku avishwa Sanda Geita


Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita RPC Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kuwepo kwa matukio ya vitendo vya ushirikina katika Kata ya Buhalahala iliyopo wilayani Geita mkoa wa Geita.

Kamanda Mponjoli amethibitisha hilo leo kufuatia tukio la hivi karibuni lililohusisha mzoga wa kuku ukiwa umevalishwa Sanda kukutwa umetelekezwa nyumbani kwa Emmanuel  Kabodi mtaa wa 14 Kambarage.

“Ni kweli matukio haya yanayohusisha imani yapo lakini hatuyapi nafasi sana labda mpaka yanapofikia hatua ya kutia hofu miongoni mwa wanajamii lakini mara nyingi huwa tunawaachia wenyewe wayatatue na sisi huingilia tu endapo yakihatarisha usalama” amesema RPC Mponjoli.

Aidha RPC Mponjoli ameongeza kuwa jeshi la polisi mkoani Geita linafuatilia tukio hilo ili kujiridhisha kama halijaleta madhara ama hofu kwa wakazi wa eneo hilo.

Hata hivyo Askofu wa kanisa la  TMRC Mkoani Geita Stephano Saguda alifanikisha zoezi la kuuchoma moto mzoga huo.

Hakuna maoni: