Jumanne, 26 Septemba 2017

VIDEO: Nyalandu ambeba Mgonjwa Mwingine kwa Ndege Singida


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Nyalandu ameandika taarifa hii

Hospitali ya Rufaa Hydom, MANYARA. (Mpakani mwa Singida na Manyara):-
NIMEWASILI uwanja wa ndege wa Hospitali ya Hyadom kwa ajili ya dharura ya kumsafirisha mgonjwa, Bw. Samson Mwanga, mkazi wa kijiji cha Mipilo, Singida Kaskazini, aishiye kijiji cha Gidika (Manyara) aliyepatwa na kupasuka MSHIPA kichwani na kusababisha kuhitaji kile MADAKTARI walichokiita 'Immunogloblin Injections" ili kunusuru maisha yake. Tumempandisha NDEGE ya Shirika la "Flying Medical Doctors", iliyotokea Nairobi na kuwasili hapa Hydom mchana huu. Nawashukuru MADAKTARI na wanafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Hydom

kwa UTUMISHI wao uliotukuka, na kwa kumhudumia mgonjwa Samson Mwanga hadi tukaweza kumpandisha NDEGE kwenda Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Kilimanjaro mchana huu. JOPO la MADAKTARI wa Kitanzania Hydom liliwahusisha Dkt. Renatus Fabiano, MD, Dkt. Benson Mwakalukwa, MD, na Dkt. Daudi Lotto, MD; na UONGOZI wa Hospitali uliwakilishwa na Ndg. Joseph Olesaiburu, Katibu wa Hospitali, Ndg. Timoth Dakai, Mhasibu, na Bibi Ruth Mneney, Muuguzi Mkuu Msaidizi. Shukrani sana kwa Kepteni Mkuu Mike ASANTENI SANA. MUNGU AWABARIKI . Shukrani kwa Mrusha ndege Capt. Mike na Uongozi wa Flying Medical Services #MunguIbarikiTanzania #HydomHospital #KCMC #SingidaKaskazini


Hakuna maoni: