Jumanne, 26 Septemba 2017

UNALIKUMBUKA LILE TUKIO LA UBAGUZI WA RANGI KWENYE NDEGE?, HABARI HII IKUFIKIE KUHUSU MUENDELEZO WA TUKIO HILO.



British Airways imeanzisha uchunguzi dhidi ya video inayomuonesha mmoja wa watumishi wake wa kike wa Ndege akitoa lugha ya kibaguzi kwa abiria wakati ndege hiyo ikifanya safari kuelekea Nigeria.
Mwanamke huyo, akiwa katika sare ya BA, alijirekodi video hiyo muda mfupi akijiandaa kwa safari kutoka Uwanja wa Ndege wa Heathrow, London kwenda Abuja, Nigeria, Ijumaa usiku ambapo video hiyo iliyorekodiwa kwenye gari ilisambazwa kwa watumishi wengine ambao walitoa taarifa kwa BA.
Leo Septmber 26, 2017 Shirika hilo limesema:”Tunatarajia weledi katika kazi miongoni mwa watumishi wetu wanapowakilisha British Airways. Tunachunguza hii video.”


Hakuna maoni: