Ijumaa, 22 Septemba 2017

MBOWE: VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAHUSIKA KUPIGWA RISASI KWA TUNDU LISSU

Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe amesema mshukiwa namba moja wa tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi ni vyombo vya.ulizni na usalama

Mbowe ameyasema hayo leo katika ofisi za CHADEMA jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia hali ya Tundu Lissu.

"Kama kiongozi wa Chama nadiriki kusema kwamba mshukiwa namba moja wa shambulio la Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii" 
.
"Hilo nalisema bila kumung'unya maneno, viashiria vyote vya tukio lile tangu linatokea kauli na kusita kwa viongozi na kauli za kujiosha.". Amesema Mbowe


Awali mbowe alisema ,kwa ujumla mgonjwa anaendelea vizuri na amemtuma awasilimie watanzania kwa niiaba yake


"Tundu Lissu anawasalimu sana. Nimeachana naye Nairobi jana mchana nikamwambia nitazungumza na Watanzania."..Amesema mbowe


Pia Mbowe alisema.taarifa za madaktari kuhusu hali ya mgonjwa ni siri, hivo inatosha lusema tu.kuwa.mgonjwa anaendelea vizuri

""Taarifa ya madaktari kuhusu hali ya Lissu imetolewa ni siri na itoshe tu kuwapa kwa upande huo."  Amesema Mbowe.



Hakuna maoni: