Lwandamina amesema kwamba Tambwe ni mshambuliaji anayejua majukumu yake vizuri na ambaye kukosekana kwake kumeipunguzia makali safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
Kukosekana kwa Amissi Tambwe wazi kumepunguza makali ya safu ya ushambuliaji ya Yanga
“Ameanza mazoezi jana, hivyo bado ni mapema kusema chochote juu ya namna alivyoimarika, anahitaji muda kidogo,”amesema Lwandamina.
Tambwe aliumia mapema Agosti katika kambi ya mazoezi kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba SC uliofanyika Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na Yanga kufungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Lakini maumivu hayo yalikuwa ni kama kutonesha maumivu yake ya msimu uliopita yaliyomuweka nje kwa muda mrefu pia.
Yanga ipo katika maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi, tayari wamekwishacheza mechi nne hadi sasa, wakishinda mbili na kutoa sare mbili, ingawa makali ya safu ya ushambuliaji yamepungua kutokana na kuvuna bao moja katika kila mchezo, sare za 1-1 na Lipuli na Maji Maji na ushindi wa 1-0 dhdi ya Njombe Mji na Ndanda FC.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni