Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi (kulia) akiwa. Anayefuata ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, Mwenyekiti wa Kamti ya Maudhui ya TCRA, Bibi Msoka na James Kilimba ambaye ni Mkurugebnzi wa Bodi ya TCRA |
Mamlaka ya mawasiliano tanzania TRA kushirikiana na mtandao wa wanablog Tanzania(TANZANIA BLOGGERS NETWORK - TBN), Leo tarehe 22 september imeandaa Warsa iliyolenga uwezeshaji kwa wamiliki na waendeshaji wa blog Tanzani juu ya matuminzi bora ya vyombo vya habari vya mtandaoni maarufu kama online media.
Awali katika warsha hiyo Thadeo Lingo Mjumbe wa bodi ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano TCRA, alianza kwa kutoa hali halisi ya matuminzi ya mtandao wa internet ulimwenguni kwa ujumla ambapo alisema
Mwanzo wa mwaka 2017 jumla ya watumiaji wa internet ulimwenguni ilifikia 3.773 bilioni ambayo inakadiriwa kua 50% ya watu wote ulimwenguni. Watu 3.448 billion waatumia internet kwa kutumia smartphone sawa na 92%.
Kwa upande wa Tanzania idadi ya watumiaji wa simu imeongezeka kutoka 25 milions mwaka 2011 mpaka 40 millions mwaka 2017.
Ameongeza kuwa idadi ya watumiaji wa mtandao wa internet imeongezeka kutoka 5millions mwaka 2011 mpaka kufikia 19 millions mwaka 2017, idadi hiyo inajumuisha watumiaji wa wireless internet 3 millions mwaka 2011 mpaka kufikia 18 millions mwaka 2017.
Washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JK Nyerere. |
Kutokana na ongezeko hilo la watumiaji wa internet changamoto pia zimejidi kuongezeka ikiwemo wizi wa kutumia mtandao na makosa mengine ya kimtandao(cyber crimes) Ameongezea Kamanda wa polisi msaidizi kitendo cha makosa ya mtandaoni ASP Joshua Mwangasa wakati akihudhurisha Mada kwa wamiliki hao wa blog.
ASP Joshua Mwangasa kulia. |
Serikali kupitia vyombo vyake mbali mbali ikiwemo Mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA na jeshi la polosi imeahidi kuendelea kutoa elimu kwa watanzania juu ya makosa ya kimtandao na namna ya kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuletea maendeleo.
Mwanzilishi na Mmiliki wa mtandao wa jamii forum, Macksence Melon akiwa kwenye warsha hiyo. |
Warsha hiyi pia imemalizika kwa uzinduzi Rasmi wa awamu ya pili ya matuminzi ya mitandao ya kijamii Ambayo imepewa kauli mbiu ya USINITUMIE, SITAKI, SIMTUMII MWINGINE, NITAKURIPOTI. Kwa ajili ya kuhamasisha jamii juu ya matumizi bora ya huduma za mitandao ya kijamii.
Wajumbe wa Warsa wakisikiliza Mada. |
Nimekuwekea hapo Video fupi ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo hapa chini unaweza kuitazama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni