Jumanne, 26 Septemba 2017

Ivory Coast: Zaidi ya wanafunzi 40 wakamatwa baada ya ghasia na jeshi la Polisi


Zaidi ya wanafunzi 40 wakamatwa kufuatia ghasia zilizozuka  baina yao na jeshi la Polisi inchini Ivory Coast

Wanafunzi 40 wamekamatwa  na kuwekwa kizuizinş mjini Abidjan kufuatia ghasia zilizozuka Juma lililpita mjini Abidjan.

Taarifa ya kukamatwa kwa wanafunzi hoa imetolewa na  muungano wa wanafunzi wa Ivory Coast FESCI.

Muunganı huo wa wanafunzi ulifahamisha katika tangazo lake kuwa  wanafunzi watatu wa kike walikamatwa wakiwa katika chumba chao na kupelekwa kizuizini.

Wanafunzi hoa waliandamana Septemba 13 na Septemba 18 wakiddai kuondolewa kwa kiwanga cha pesa  kilichoongezwa katika ada.

Muungano huo umefahamisha kuwa umeandaa maandamano mapya ili wanafunzi wenzao waliokamatwa wachwe huru.

Hakuna maoni: