Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Muleba imekamata tani 19 za samaki aina ya sangara wenye thamani ya Sh57 milioni ambao wamevuliwa kinyume cha sheria katika vijiji vilivyopo kisiwa cha Mazinga wilayani humo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba, Benjamini Mwakisyege amesema hayo hii leo Jumamosi Januari 13 wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kamati hiyo kukamata tani 7 za samaki wa aina hiyo wenye thamani ya Sh21 milioni siku ya Jumatano Janauari 10 kutoka kisiwa hicho cha Mazinga na maeneo mengine wilayani humo waliovuliwa kwa njia haramu.
Mwakisyege amesema leo Ijumaa kamati hiyo pi ilikamata samaki tani 12 wenye thamani ya Sh36 milioni katika kijiji na kata ya Kagoma na kwamba samaki hao wanavuliwa kwenye vijiji vya kata hiyo na kutoka visiwa vya Bumbire
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni