Jumamosi, 18 Novemba 2017

Watanzania zaidi ya 40 wafanyiwa upasuaji moyo bure

Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na wenzao kutoka Saudi Arabia wamefanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo  zaidi ya wagonjwa 40.

Kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya kiislamu ya misaada IIRO kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji kwa kutumia mtambo wa Cathlab ambao ni wa kuzibua mshipa ya damu bila wa mkono bila kufungua kifua.

Aidha upasuaji huo uliofanywa katika hospitali ya Muhimbili tangu november 15 hadi 18 mwaka huu umekuwa na faida ya kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaruhusiwa  tofauti na upasuaji wa kutumia mishipa ya paja ambao ulikua unatumika, ambapo mgonjwa lazima akae hospitali zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo yake.

Sambamba na huduma hiyo  madaktari hao kutoka Saudi Arabia walikua wakitoa elimu na kubadilishana ujuzi wa kazi kati ya taasisi hizo mbili ikiwemo aina mpya ya upasuaji uliofanyika ambapo umewajengea uwezo pia wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na uzoefu mpya wa baadhi ya magonjwa na teknolojia ambayo katika nchi yetu hamna.

Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi JKCI Doct. Peter Richard amewashukuru kwa ujio wao kwani wameokoa fedha nyingi ambazo watanzania wlitakiwa waende kutibiwa nje.

Hivyo kwa namna moja na nyingine tunaishukuru taasisi ya Kimataifa ya kiislamu ya misaada IIRO kwa kutuma wataalamu wake wa magojwa ya moyo kuja kutibu hapa nchini, alisema





Hakuna maoni: