Watu wawili wamefariki dunia huku wengine zaidi ya arobaini wakiwa wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi aina ya Fuso yenye namba za usajili T 606 CTY ya kampuni ya Kisumapai linalofanya safari zake kati ya Songea, Mbinga na Nyasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi amethibitisha kutoa kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu wawili wamefariki hapo hapo huku majeruhi wengine wakiwa wamepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu.
"Gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na dereva Ismail Mohamed Nasoro ilianguka na kupoteza maisha ya watu wawili hapo hapo, huku watu 42 wakiwa wamejeruhiwa mpaka sasa jumla ya majeruhi 33 kati yao walipata matibabu na kuhurusiwa na wengine 9 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga, Mbuyura" alisema Gemini
Baadhi ya majeruhi wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva pamoja na bus hilo kuwa limebeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wake
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni